Gurudumu la Uchumi

Gurudumu la Uchumi

Fahamu masuala kadha wa kadha kuhusu uchumi kama vile, namna ya kupambana na umaskini, mfumuko wa bei, kushamiri kwa matumizi ya dola na athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika. Mada hizi zinafanyiwa utafiti wa kina na zinazungumzwa kwa lugha rahisi inayoeleweka ili kukufanya uelewe na usichoke kusikiliza .

00:00
00:00

Episode's summary

Mji wa Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, unaendelea kukabiliwa na changamoto za kiusalama na kiuchumi, huku ukiwa chini ya udhibiti wa waasi wa FRN wanaoongozwa na rais wa zamani Josephu Kabila, ambako fursa za ajira ni chache na vijana wengi wanakabiliwa na changamoto ya kujipatia kipato, hata hivyo baadhi yao wameamua kutafuta njia mbadala za kujikimu na kusaidia familia zao.

Episodes

315-

DRC: Ufugaji wa nyuki unavyokwamua maisha ya raia wa mji wa Goma

Mji wa Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, unaendelea kukabiliwa na changamoto za kiusalama na kiuchumi, huku ukiwa chini ya udhibiti wa waasi wa FRN wanaoongozwa na rais wa zamani Josephu Kabila, ambako fursa za ajira ni chache na vijana wengi wanakabiliwa na changamoto ya kujipatia kipato, hata hivyo baadhi yao wameamua kutafuta njia mbadala za kujikimu na kusaidia familia zao.

21 Oct 2026
314-

Afrika kuzindua taasisi ya ukadiriaji mikopo, je itasaidia?

Afrika imezindua rasmi Wakala wa Ukadiriaji wa Mikopo wa Afrika, Africa Credit Rating Agency (AfCRA), hatua inayolenga kushughulikia changamoto za gharama kubwa za mikopo na kuvutia uwekezaji zaidi kwa ajili ya maendeleo ya bara hilo. Je, kuanzishwa kwake kutapunguza kweli gharama za mikopo kwa mataifa ya Afrika, au ni mwanzo tu wa safari ndefu ya mageuzi ya kifedha?

14 Oct 2026
313-

Je, Afrika itapata sauti inayodai katika uchumi wa dunia?

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, nchi nyingi za Afrika zinakabiliwa na mzigo mkubwa wa madeni na gharama za juu za kukopa katika masoko ya kimataifa. Fedha nyingi ambazo zingetumika katika afya, elimu, miundombinu na ajira zinaishia katika kuhudumia madeni, hali inayoweka shinikizo zaidi kwa uchumi wa nchi hizi. Je, hitaji la Afrika la kuwa na mfumo mpya wa kifedha duniani wenye uwakilishi na usawa zaidi litawezekana?

07 Oct 2026
312-

Kiwanda cha kusafisha mafuta Lamu: mwanzo wa mapinduzi ya nishati Afrika Mashariki?

Kenya inaagiza karibu mahitaji yake yote ya bidhaa za Petroli kutoka nje, hii ikiwa na maana kuwa bei na upatikanaji wa mafuta katika nchi hii, na kwa kiasi kikubwa katika ukanda unaweza kuathiriwa na mambo yanayotokea katika masoko ya kimataifa, hata hivyo habari njema ni kuwa bilionea wa Afrika Aliko Dangote anajenga kiwanda cha kusafisha mafuta huko Lamu. Kwanini hatua hii ni muhimu? Tufuatilie

30 Sep 2026
311-

Hormuz na Bab el-Mandeb: Njia za baharini zinazotikisa uchumi wa dunia.

Msikilizaji hebu fikiria mafuta unayoweka kwenye gari lako, bidhaa zinazofika kwenye maduka yetu kutoka Asia, mbolea inayotumika kwenye kilimo, au hata gharama ya kusafirisha kahawa na chai kutoka Afrika kwenda masoko ya nje, kwa namna moja au nyingine, sehemu ya uchumi huu inategemea bahari na kufungwa kwa njia ya Hormuz na sasa ile ya Bab el-Mandeb kunauweka uchumi wa dunia hatarini. Ungana nami kwenye makala ya wiki hii kufahamu zaidi.

23 Sep 2026